Ikiwa umitimia mwaka mmoja sasa toka harakati za wana yesu okoa mitaa YOM kuanzishwa moja ya mafanikio tuliyo yapata ni kuokolewa kwa watu sehemu mbalimbali sababu ikiwa ni kwa huduma yetu ya uimbaji, haya yamesemwa na mmoja wa wanaharakati ambao hasa ndio mstari wa mbele kuhakikisha kwamba shetani ana kula za uso mpaka ana sanda, jumapili ya tar 24 augost 2014. tulikua tunatimiza mwaka mmoja toka kuanzishwa kwa huduma yetu ambayo kimsingi imefanikiwa saana kwasababu tumekua na wadau ambao wana tu surpot sana iwe kwa hali na mali, hatuwezi kuwataja wote wanao tu surport lakini Mungu anawajua na tunawaombea saana, lakini nitoe shukrani zangu nyingi kwa niaba ya wana YOM wote kwa mh:Katibu mkuu wa TAG Rev Roni Swai ambae pia ndio mlezi wetu, kwa. lakini Mungu ni mwema saana kwani mtumishi wa Mungu COSATO CHUMI kwani alitufanyia surprise ya kutuzawadia camera aina ya SONY {div}cam yenye thamani ya Tsh 12,000,000/= milioni kumi na mbili. ilikua shangwe na vigeregere saana. hayo yalikua maelezo ambayo ali tiritirika Mtumishi wa Mungu RUNGU LA YESU pale nilipo fanya na e mahojiano, aliendelea kwa kusema kwasasa tumefikia sehemu nzuri saana tafauti na mwanzo ambapo watu wengine walikua wakibeza huduma yetu lakini sasa unaona Mungu wetu anajibu maombi yetu kwa sababu kupata camera hii ndio mwanzo wa kufikia malengo yetu ya kufikisha huduma yetu mbaali zaidi, kwa hiyo kwa sasa ni kazi kwetu kufanya Audio songs nzuri zenye ubora na baadae kufanya video ambapo tayari camera tunayo ooooh haleluyaaaa! alisema. Mwisho akasema watu wanatakiwa wajue kwamba YOM sio ya mtu fulani YOM ni ya kila mtu anae mjua Mungu na yupo tayari kumtangaza yesu kwa njia ya uimbaji film n.k kwani kwa sasa mpango wetu ni pamoja na kufanya film kwahiyo kwa yeyote atakaye hitaji kufanya kazi na sisi iwe song video au film awasiliane kupitia blog hii au tembelea ukurasa wetu wenye jina la YESU OKOA MITAA TZ. ASANTE.
Kamera iliyo tolewa
Masanja pia alikuwepo kutoa surport
Rungu la yesu akishukuru kwa niaba ya wana YOM
Emmanuel mbasha pia alikuwepo.
Masanja kama kawaida yake .. akifanya yake
Mlezi wa YOM mtumishi SWAI.
0 comments
Post a Comment