Tuesday, March 25, 2014

SOMA HAPA UZEMBE WA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJIRI.......

Utafiti ukiwa unaonyesha kua waimbaji wengi wa nyimbo za injiri mpaka leo hawasajiri nyimbo zao cosota kitu kinacho fanya mapato yao kuwa sio mazuri unaweza kuona mwimbaji ana jina kubwa lakini kipato chake ni kidogo saana ukilinganisha na jina lake kua kubwa.inasemekana mara nyingi wasambazaji huuziwa kazi ikiwa master na msambazaji ndie husajiri kazi ile kama yake. ambapo msambazaji huyo atakua na haki kwa 100% kwenye kazi hiyo.
 mfano ukimuuzia album yako msambazaji yeye anaenda kuisajili kama yake yaani mali yake anaimiliki kwa kila kitu na warithi wa kazi hiyo yeye huandika watoto wake, pata picha wewe umerecord
 album ya gospel unapewa mil 8 au 10. lakini unakua huna haki tena ya nyimbo hizo msambazaji anauwezo wa kuzipeleka ring tone, kule push mobile na sehem nyingine akawa analipwa yeye hela. na tatizo jingine ni baadhi ya waimbaji hukumbuka kusajili kazi zao lakini hawaendi kwenye kampuni za kufanya milio ya mpigaji, ambapo nyimbo zako zikiwa kule huweza kukuingizia kipato
kulingana na umaarufu wa nyimbo zako, maana yake hicho pia ni kipato, kinacho weza kukusaidia kukupa mapato kuliko kusubiri uitwe sumbawanga ukaimbe kwenye tamasha na ulipwe laki 3 au 4, isipotokea je? sisi kama wamiliki wa blog hii tumeamua kutoa ushauri na maelekezo ya jinsi ya kufanya mambo hayo mawili kusajili nyimbo COSOTA. na kuweka nyimbo kua MLIO WA MPIGAJI. wasiliana nasi kwa number hii
{0714 045 080}.

0 comments

Post a Comment