Taswira ya picha za jehanam
Taswira
Taswira
IKIWA BABU YANGU ALIYE MZAA BABA ANGU ANA USHUHUDA KAMA HUU ILA NIPO KATIKA MAANDALIZI YA KUTENGENEZA MAKALA ITAKAYO KUJIA HAPAHAPA ILA LEO NAKUOMBA SAANA TUMIA MDA WAKO KIDOGO KUSOMA USHUHUDA HUU UTAKUFANYA UJIFUNZE KITU KIKUBWA SANA KARIBU.
KUITWA:
Ilikuwa ni mwezi wa 12/1991 tulipochaguliwa vijana 10 kuombea Mkutano wa
Kiroho ambao ulikuwa ukifanyika pale Uyole. Siku moja baada ya maombi
ya usiku, nilala pamoja na dada zangu. Siku hiyo nilala usingizi mzito
ambao sijapata kuona. Usiku nilishangaa kukuta usingizi umetoweka
kabisa, hivyo nikabaki nikiwa macho, ndipo nikasikia sauti ikiita
‘Nyisaki’ nikasikia lakini sikuitikia, ikaita mara ya pili pia
sikuitika. Hata mara ya tatu ndipo
nikaitika kisha nikasikia ile sauti ikisema Nimekuchagua kuwa mtumishi
wangu ndipo nikatambua kuwa ni sauti ya Bwana, nikasema Bwana mimi ni
mtoto mdogo tena hata chuo chochote sijaenda nitawezaje kuifanya kazi
hiyo? Bwana akaniambia mkumbuke Yeremia mtumishi wangu nilimchagua
angali bado mdogo (Yeremia 1:5) basi nikaendelea kubishana na ile sauti
hadi dada yangu mmoja aliamba na kusema Mshukuru Mungu kwa sababu
amekuchagua wewe.
Ndugu msomaji kumbuka kuwa sauti hiyo nilisikia nikiwa macho kabisa na
wala haikuwa ndoto na baada ya kusikia sauti hiyo mara ya pili na ya
kwanza niliamka na kuthibitisha kabisa kuwa wote niliokuwa nimelala nao
bado wamelala. Na hata huyo dada yangu alisema ‘Mshukuru Mungu kwa
sababu amekuchagua wewe, nilitambua kuwa ni Mungu ndiye aliyemuelimisha
na kumfunulia jambo hili. Baada ya yote haya tukamshukuru Mungu na
kulala.
Kesho yake tarehe 30/12/1991 ndipo nilipoonyeshwa mambo makuu ya ajabu (Yeremia 33:3)
JEHANAMU
SEHEMU YA KWANZA NA MANGOJEO YA WAFU:
Ikiwa tarehe 30/12/1191 tulipoamka tukaenda kwenye semina na baada ya
ile semina tuliamua kwenda kumuona rafiki yetu aliyeokoka ambaye kwa
muda ule alikuwa hajiwezi yaani alikuwa anaumwa. Tulipofika pale
nyumbani tukafungua ibada kwa maombi kisha tukaanza kujifunza jinsi
Biblia inavyosema kwa njia ya maswali. Hata baada ya hapo tukaamua
kufunga Ibada kwa maombi kama tukivyofungua. Tufunge kwa maombi na
kumkabidhi ndugu yetu mikononi mwa Bwana, maana tulianza ibada yetu kwa
kumshukuru Mungu kwa kuwa ndugu yetu alikuwa hajamboâ Ninachokumbuka ni
kwamba tuliimba pambio moja ya kuabudu lakini sikumbuki kwamba tuliingia
kwenye maombi au la tulipokuwa tunaimba ile pambio ya kuabudu,
nikashangaa kuona kuwa nimechukuliwa niko sehemu tofauti kabisa na
mazingira ya nyumbani.
Ukiniuliza kuwa nilichukuliwa vipi hata mimi mwenyewe sielewi, lakini
nilishangaa kuona kwamba niko kwenye bonde moja kubwa sana, na lile
bonde lilikuwa halina miti wala majani wala ndege na vitu vilivyopo
duniani, sehemu yenyewe ilikuwa haivutii hata kidogo, ni sehemu moja
iliyokuwa na ukimya wa aina yake. Sasa nikashangaa mbona nilikuwa na
rafiki zangu na sasa siwaoni, nikaendelea kujiuliza ni nani aliyenileta
huku, na hapa ni wapi? Basi niliamua moyoni mwangu kuwa liwalo na liwe
kwa sababu sijui hata aliyenileta mahali hapa, nilikuwa nimekata tamaa,
nikajiandaa kutaka kukaa ndipo nikasikia sauti nyumba yangu ikisema
Nyisaki nifuate.
Nilipoinuka nilishangaa sana kumuona mtu mmoja mfano wa mwanadamu
nilipomtazama yule mtu, umbo lake hakuwa mrefu sana wala hakuwa mnene
sana, alikuwa ni mtu ambaye sijawahi kumuona popote duniani. Nywele zake
zilikuwa ndefu na alikuwa amezibana nyuma kwa banio jekundu, alikuwa
amevaa vazi refu mpaka miguuni na jeupe sana ambalo hata weupe wake
sijawahi kuuona hapa duniani. Alikuwa ni mweupe sana, siyo weupe wa hapa
duniani, macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, huyo mtu alikuwa
hakanyagi chini bali alikuwa akitembea hewani na vazi lile lilikuwa
liking'aa sana haliwezi kabisa kutazamika kwa macho ya binadamu.
Nayasema mambo ambayo niliagizwa niyaseme, huyu mtu alikuwa amejifunga
mkanda mmoja mwekundu kiunoni ndipo nikaamka nikaanza kumtuata. Baada ya
hatua chache nikaanza kusikia muungurumo Fulani ambao ulinitisha kwa
kiasi Fulani lakini sikuuliza. Kadiri tulivyozidi kutembea mbele ndivyo
muungurumo ulivyozidi kuongezeka na kutisha zaidi, mara nikasikia sauti
yangu ikiniambia inua macho na tazama mbele, ndipo nikashituka sana
nilipoona moshi mkubwa mnene na mweusi umefunika bonde lile na
kusababisha giza nene katika bonde. Nikamuuliza yule mtu huko mbele kuna
nini? Yule mtu akasema, hiyo ni Sehemu ya Jehanamu watakakoenda watenda
dhambi baada ya maisha ya duniani.
Baada ya kusikia hayo yote ndiyo nguvu zikaniishia, nikaanza kulia na
kumuomba sana Mungu anisamehe maana kwa mawazo yangu nilifikiri nimekufa
na sasa napelekwa Jehanamu nikaendelea kulia sana hadi yule mtu
aliponieleza usilie maana ukilia utashindwa kuwafikishia watu wangu
habari hizi. Hofu ilijia nilitishika mno, lakini mpango wa Mungu
kunionyesha mambo haya ni kuwaambia watu. Ndugu msomaji, kweli Jehanamu
ninavyoelezwa kuwa ni ziwa la moto elewa hivyo. Nilipotazama sikuona
mwisho wake, bali niliona milipuko mikubwa sana na ya kutisha na
milipuko hiyo haikufanana na milipuko yoyote hapo duniani labda kwa
sehemu inayoweza kulinganishwa na milipuko ya visima vya mafuta.
Milipuko hiyo ni mikubwa na inatisha mno iliyosababisha moshi mkubwa
sana ulioambatana na moto wa kupaa juu. Moto ule ulijichanganya
changanya kama vile bahari iliyochafuka. Kulikuwa na mawimbi makubwa na
ya kutisha na yakichanganyika na kutoa miungurumo mikubwa ambayo haiwezi
kumfanya mwanadamu kusikia hata mateso ya mwenzake. Mimi nilipokuwa
nasikia habari ya Jehanamu nilifikiri labda ni moto mdogo au makaa ya
moto. Lakini siku hiyo niliyoona mwenyewe kiasi kwamba nilibaki kulia na
kuomboleza kwa uchungu mkubwa mno. Mtu yule alifanya kazi ya kunionya
nisillie, pia alinitia nguvu na ndipo nilipoweza kuendelea, ndugu yangu
ukisikia Jehanamu iogope kama ulivyo.
Nilipoangalia ndani ya ule moto niliona vitu vyenye uhai virefu vyeupe
nikauliza hivyo ni vitu gani? Yule mtu akasema hao ni funza wa Jehanamu
hizo rangi kwenye pingili zake ni za nini? Akasema hivyo siyo rangi,
kama unavyowaona hao funza wana meno hayo manne yenye uwezo hata wa
kutoboa fuvu la kichwa cha mtu, na huyo funza akishaingia ndani huacha
sumu kali yaani hiyo unayoiona kama rangi ambayo humtesa mwanadamu
milele na milele. Hao funza walikuwa ni wengi sana lakini hawafi ndani
ya ule moto, (Marko 9:45-46) walikuwa wembamba warefu yapata mita moja,
na walikuwa
na pingiri pingiri ambazo zilionekana kuwa na rangi, walikuwa na meno
mawili mbele na kichwani kulikuwa na meno mawili jumla ya meno yote
manne, yaani mkiani na kichwani kulikuwa na midomo.
Bwana akasema hawafi wala hawaugui kwa sababu wamehifadhiwa kwa ajili ya
mateso ya watenda maovu Ndugu msomaji, nisingeweza kupoteza muda
wangu kukuletea jambo ambalo sijaliona lakini nimesema haya ili ukiwa na
masikio na uyasikie, ukikataa ni juu yako mwenyewe. Maana sikuambiwa
kwamba nimlazimishe mtu aokoke, bali niliambiwa nikamwambie kila mtu
labda atakuwepo mmoja atakayegeuka na kuponywa. Sasa nikauliza mbona
watu wanasema Jehanamu kuna wanaoungua lakini iweje Jehanamu hii haina
watu wanaungua? Akasema wanasema kweli lakini watu watakuja kutupwa kwa
wakati wake. Lakini muda huu wamehifadhiwa wakimsubiri baba yao
aliyewadanganya (yaani shetani).
Akasema twende nikakuonyeshe nikaanza kumfuata. Kweli ndugu zangu
Jehanamu uisikie kama ilivyo. Nilipofikiri habari za wale funza wa ajabu
kwa kweli nililia kwa uchungu mkubwa mno nilitetemeka na kuishiwa nguvu
nikaanza kuwaza moyoni mwangu mtu anayejua dhambi ni mbaya, na anajua
neema ya Mungu na kupuuzia kweli uje kuteswa katika ziwa hili la kutisha
lenye moto usiozimika na funza ambao hawafi, kwa kweli nililia sana.
Lakini yule mtu akaniambai nyamaza, maana ukilia utashindwa kuyafikisha
yote ninayotaka kukuonyesha. Kwa kweli nashindwa hata nieleze vipi.
Jehanamu ni kweli ipo na inatisha sana; achana na mafundisho ya
mashetani yanayosema hakuna Jehanamu na ukiendelea kufuata hayo
utaangamia na kujuta milele.
Ninaeleza ndugu yangu kuwa Mungu hapendi upotee ndiyo maana amekupa
nafasi kama hii. Nayo yawezekana ni nafasi ya mwisho sasa usipokubali
kutubu yawezekana ukajiletea maangamizi wewe mwenyewe.
JEHANAMU
IMEANDALIWA KWA AJILI YA SHETANI NA MALAIKA ZAKE:
Niliondoka sehemu hii ya Jehanamu na kuelekea sehemu ya mangojeo nikiwa
nalia kwa uchungu mkubwa mno. Na haya ninayokuambia sikutishi bali
nakuambia kweli na kama unafikiri nakutisha basi utakwenda kuona
mwenyewe. Nikaenda kumfuata yule mtu, tulipofika mahali fulani na
kutazama bondeni niliona bonde kubwa lililokuwa limefunikwa giza la
kutisha mno.
NB: ushuhuda huu usitufanye tuegemee kwenye imani moja.... ukristo na uislamu wote unaamini kuwepo kwa jehanamu..
Thursday, April 3, 2014
IKIWA WEWE NI MKRISTO AU MUISLAM JEHANAMU UNAIJUA?? SOMA HAPA KWA UTULIVU.......
Posted by
Unknown
at
2:30 AM
Tags :
0 comments
Post a Comment