ROSE MUHANDO KATIKA POZI |
Ile habari iliyoandaikwa na Moja ya magazeti yanayotoka mara moja kwa wiki kuwa muimbaji wa nyimbo za Injili Rose Muhando alifikishwa kituo cha polisi kwa utapeli, sasa ukweli wake wajulikana.
Akizungumza na Mtandao wa MO Designtz, Producer au mtayarishaji wa muziki anayetengeneza nyimbo za Rose Muhando Enock Nyongoto au Producer Eck, amesema kuwa Rose Hajafikishwa kituoni ila yeye ndiye aliyekwenda kituoni na si Rose.
PRODUCER ECK AKIFANYA MAMBO YAKE |
akihadidhia kisa kizima kilivyokuwa Producer Eck alisema kuwa Baada ya Rose kukabidhiwa pesa kwa makubaliano ya kwenda kuimba huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mji wa Bunia, Rose alijikuta akiwa na wakati mgumu sana kwani Kampuni anayofanya nayo kazi ambayo ni kampuni ya Msama Promotion walikuwa tayari walishaandaa matamasha na ambayo yalikuja kwa kufuatana hivyo akajikuta kuwa yale maandalizi tu yanaingilia ratiba zingine zote kwa vile alitakiwa kufanya mazoezi mazito kwa ajili ya kuimba live. akaendelea kusema kuwa mazoezi hayo yalikuwa mazito kwani Rose hakuwahi kuimba live hivyo akajikuta ana kazi kubwa ya kufanya mazoezi na wanamziki watakaompigia live hivyo hakuweza kabisa kwenda Congo na ukizingatia kuwa Pesa waliokubaliana na huyo Mchungaji wa Congo haikutolewa hata nusu yake.
Produce Eck anasema kuwa, Rose na huyo Mcgungaji walikubaliana kiasi cha Dola za kimarekani 5,000$ ambayo ni sawa na Shilingi milioni 8 lakini alipewa advance ya shilingi milioni 3.
MKURUGENZI WA KAMPUNI YA MSAMA PROMOTION ALEX MSAMA |
Eck anasema kuwa Rose hakufanya makusudi na wala hakuwa na nia ya kufanya kama ilivyotokea. na hizi habari zilizoandikwa ni za upande mmoja kwani Rose alipokuwa akipigiwa simu alikuwa kwenye tamasha Mwanza na mara nyingi akiwa kwenye tamasha huwa hakai na simu yeye, simu wanakuwa nayo vijana wake.
ROSE MUHANDO KATIKA VIDEO YAKE YA WOLOLO |
Producer Eck anaendelea kusema kuwa Msama hakusema uongo kwani leo baada ya kufika uwanja wa ndege tu kutoka Mwanza, Msama alimpigia simu Producer Eck na akamuambia akachukuwe pesa hiyo ili walipe wamalize hilotatizo. " kweli Msama alipofika tu kabla hata hajafika nyumbani kwake, alinipigia simu na kuniambia nikachukue pesa hizo kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo. Nami nilimpigia simu mchungaji tukaenda kuchukuwa hizo pesa kisha tukaenda kituo cha polisi pamoja na mchungaji kwa ajili ya kufuta jalada. hivi unavyoniona ndio nimetoka huko kituo cha polisi kwa hiyo hakuna kesi tena, na mchungaji kati ya kesho au keshokutwa anaondoka. alimalizia kusema Producer Eck.
PRODUCER ECK AKIWA NA MUIMBAJI CHIDUMULE |
Naye Rose Muhando akizungumza na MO Designtz, amesema kuwa anafahamu kuwa mashabiki wake walioko Bunia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wana hamu sana ya kumuona, hivyo anafanya mpango lazima aende kwa ajili yao na anawapenda sana.
0 comments
Post a Comment