IMANI.
Neno "IMANI" ni neno jepesi sana kulitamka na kuliandika lakini lina maana kubwa sana katika ulimwengu wa roho. Neno hilo lina maana ya "TUMAINI" au "TEGEMEA". Ili mtu aweze kuamini, ni lazima awepo yule ambaye anaaminiwa. Haiwezekani mtu akaamini pasipo kuwepo yule anaye aminiwa. Ili imani hiyo iwe imara na isiyo teteleka ni lazima mtu yule anaye amini awe na uelewa mkubwa na wa kutosha kuhusu yule ambaye anamwamini.
Mpendwa msomaji, hebu nikuulize swali; Je! Wewe unamjua na kumfahamu yule unaye mwamini?
Swali hilo ni la msingi sana katika kufahamu imani ya kweli. Watu wengi wamejikuta wakiamini mahali ambapo hakuna tumaini la kweli, wakitumaini mahali ambapo hakuna msaada, na matokeo yake wanakuwa wanaangamia taratibu pasipo wao kujitambua.
Swali hilo ni la msingi sana katika kufahamu imani ya kweli. Watu wengi wamejikuta wakiamini mahali ambapo hakuna tumaini la kweli, wakitumaini mahali ambapo hakuna msaada, na matokeo yake wanakuwa wanaangamia taratibu pasipo wao kujitambua.
Katika "IMANI", hakuna jambo baya kama kukosea kuamini. Kwa
maana mtu anapo aminishwa vibaya anakuwa amefungwa katika fahamu zake
ambapo anakuwa amejengewa tabia ya kumtegemea yule ambaye ndani
yake hakuna tumaini la kweli wala nguvu na uweza wa kutoa msaada katika
kila hitaji.
Basi, neno IMANI maana yake ni:
Basi, neno IMANI maana yake ni:
"...imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana." (Waebrania 11:1)
Hivyo basi; mtu anaye amini ni lazima awe na
uhakika wa kile anachotegemea kukipata, na ili awe na uhakika wa
asilimia zote ni lazima mtu huyo awe anamfahamu na kumjua vizuri yule
ambaye anamwamini (anaye mtegemea kumpatia na kumtimizia mahitaji yake). Na hapo ndipo hiyo inakuwa ni "imani ya kweli".
Biblia takatifu iliposema "...imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo..." inamaanisha
kwamba; hapo hakuna kukisia wala kuwa na mashaka. Unapokuwa na imani au
unapotamka neno la imani; mfano, unapotamka neno la uponyaji kwa
mgonjwa au mtu asiye jiweza, haupaswi kuwa na mashaka mashaka wala hofu
juu ya uponyaji wa yule mgonjwa. Unapaswa kuwa na uhakika kwamba mgonjwa
yule ameshapokea uponyaji, na mgonjwa naye pia anapaswa kuamii kuwa
yeye amekwisha pona hata kama hali yake ya mwili wake yaonekana bado ni
dhaifu kwa macho ya asili.
Najua hapa kwa mtu wa mwilini ni vigumu kuelewa kwa wepesi, lakini
usihofu, fatilia kwa makini somo hili nawe utaelewa na kubarikiwa kwalo.
MTAZAMO WA KIDUNIA.
Katika dunia hii tunayo ishi yapo matabaka makuu mawili ya imani, nayo ni kama ifuatavyo:
i/: Imani ya Uongo ; ii/Imani ya Kweli.
i/: Imani ya Uongo ; ii/Imani ya Kweli.
Matabaka hayo mawili ya imani yote yanapishana katika misingi ya imani
ingawa yote yanamfundisha mtu ajenge tumaini kwa yule wanaye mtegemea.
Yote yanasema yanamwongoza mtu katika njia impelekayo mahali salama
japokuwa yote mawili yanapingana ki-mafundisho.
Baada ya kufahamu hayo itakuwa vema tujifunze kuhusu msingi wa imani
moja baada ya nyingine katika hayo matabaka mawili ya imani, kisha ndipo
tujifunze namna ya kutofautisha imani ya kweli na imani ya uongo. Hebu
tujifunze ifuatavyo:
Tunapojifunza swala zima la IMANI ni lazima tulitazame kwa mtazamo mpana na wa kina, kwa sababu ndani yake tunakuta upo mchipuko wa makundi makuu manne yasiyo endana. Kundi la kwanza ni la watu wale wanaosema kuwa "hakuna Mungu"; Kundi la pili ni la watu wale wanaosema "yupo Mungu" ingawa hawana uhakika ni Mungu yupi anaye stahili kuabudiwa; Kundi la tatu ni la watu wale wanaosema wanaye mmoja wamwabuduo lakini wakidhani wanamwabudu Mungu wa kweli kumbe wamepotea na wanazidi kupotea kwa kutoijua kweli; Kwa ujumla wao hawa wote ni watu wasiomjua Mungu aliyefanya mbingu, nchi na vitu vyote vikawepo. Lakini; Kundi la nne ni la watu wale wamwabuduo Mungu wa kweli, na wanaifahamu kweli. Je! Wewe upo katika kundi lipi kati ya hayo manne?
Yawezekana wewe haujitambui upande ulipo, sasa andaa fahamu zako na akili yako katika kuupokea ukweli huu. Zingatia kwamba: Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapo ikubali kweli. Napenda tujifunze ifuatavyo:
a): Kundi la watu wale wanaosema hakuna Mungu:
- Watu hawa huwa hawana utaratibu wa ibada wala kusanyiko. Wao
huamini kwamba maisha yalikuwepo tu, ulimwengu ulikuwepo tu na
wala hakuna aliye umba cho chote. Pia wanaamini mtu akifa hupotea tu na
kutoweka, wala hakuna kiyama cha wafu wala ufufuo wa wafu. Watu hawa
wapo wapo tu, na wala hawana mwongozo wa maandiko matakatifu; bali wao
huishi jinsi wajisikiavyo ilimradi mtu mwenyewe aona atendalo ni jema
kwake kwa kulifanya.
Lakini kwetu sisi tunaoamini uwepo wa Mungu, tunaona maandiko matakatifu yanatuambia kwamba:
Lakini kwetu sisi tunaoamini uwepo wa Mungu, tunaona maandiko matakatifu yanatuambia kwamba:
"Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema." (Zaburi 14:1)
Hivyo basi; mtu asemaye hakuna Mungu, mtu huyo ni "mpumbavu", na pia anakuwa anafanya chukizo kwa kumkataa Mungu aliye muumba.
Yawezekana umewahi kukutana na mtu mwenye imani hii, au na wewe ni mmoja
ya watu wenye kuamini hivyo. Ndugu, tambua kuwa umepungukiwa vitu vingi
ambavyo unapaswa kuvifahamu na kuwa navyo katika uelewa wako; ila
usikate tamaa na kujiona kama mtu aliye kataliwa. Sikulaumu kwa kuwa
umeamini hivyo kwa sababu uliaminishwa vibaya. Leo hii ninao ujumbe kwa
ajili yako, usemao, "toka hapo ulipo, funguka fahamu zako kwa kuwa yupo Mungu mwenye nguvu na uweza wote."
Baada ya kundi hilo la "WAPUMBAVU WASEMAO HAKUNA MUNGU", ndipoyanafuatia makundi yafuatayo ambayo ndani yake ndimo kumezaliwa neno "DINI" na "DHEHEBU / MADHEHEBU".
Tukianza na ufafanuzi: Neno DINI linatokana na asili ya lugha ya Kiarabu ambalo kwa Kiswahili chepesi neno DINI maana yake ni NJIA (way - kwa Kiingereza). Na pia; Neno DHEHEBU maana yake ni kundi la watu wa imani fulani.
Baada ya ufafanuzi huo, hebu tuendelee kujifunza ifuatavyo:
Baada ya kundi hilo la "WAPUMBAVU WASEMAO HAKUNA MUNGU", ndipoyanafuatia makundi yafuatayo ambayo ndani yake ndimo kumezaliwa neno "DINI" na "DHEHEBU / MADHEHEBU".
Tukianza na ufafanuzi: Neno DINI linatokana na asili ya lugha ya Kiarabu ambalo kwa Kiswahili chepesi neno DINI maana yake ni NJIA (way - kwa Kiingereza). Na pia; Neno DHEHEBU maana yake ni kundi la watu wa imani fulani.
Baada ya ufafanuzi huo, hebu tuendelee kujifunza ifuatavyo:
b): Kundi la watu wale wanaosema yupo Mungu ingawa hawana uhakika ni Mungu yupi anaye stahili kuabudiwa.
- Hii ni imani ambayo watu hawa wanaamini na kuabudu kitu cho chote
ambacho wanahisi yawezekana zipo nguvu ndani yake zinazoweza kuwa msaada
kwao. Watu hawa wanaamini yupo Mungu wa bahari awezaye kutuliza dhoruba
na majanga mbali mbali baharini; Wanaamini yupo Mungu wa upepo awezaye
kutuliza vimbunga na dhoruba ziletazo uharibifu zitokanazo na upepo;
Wanaamini yupo Mungu wa mvua asababishaye mvua inyeshe na kuepusha
majanga yatokanayo kwa mvua; n.k. Nao huamini kila kitu kina Mungu wake
anayejitegemea binafsi, na hao Mungu wote wanastahili kuabudiwa.
Kwa ujumla watu hawa huabudu kitu cho chote kile ambacho wao
wanadhani ndani yake kunaweza pakawa na nguvu fulani inayoweza kuwa
msaada kwao. Mfano mzuri wa watu hawa tunausoma katika Biblia Takatifu
kwenye kitabu cha MATENDO YA MITUME 17:16,22-23.
Biblia Takatifu inasema kwamba:
Biblia Takatifu inasema kwamba:
"Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake... Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, ...ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini. Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada zenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubiri habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua." (Mdo 17:16,22-23)
Biblia Takatifu inatufundisha kwamba; mji wa Athene ulikuwa umejaa
sanamu za miungu mbali mbali ambazo wenyeji wengi wa mji ule walikuwa
wakiziabudu. Watu wa Athene walikuwa wadadisi sana juu ya mambo ya dini.
Walikuwa wanaamini kuna aina nyingi za miungu ambao wote wanastahili
kuabudiwa. Ilikuwa ni makosa kwao kutomwabudu mungu wa namna yeyote ile.
Watu hao walidhani miungu wao wote ni Mungu, hadi wakafikia hatua ya
kujenga madhabahu waliyoiandika "...KWA MUNGU ASIYEJULIKANA..." Watu hao walidhani yawezekana yupo "MUNGU" mwingine anayestahili kuabudiwa ambaye wao hawamjui. Walifanya hivyo kwa kuwa hawakutaka kumuudhi wala kumchukiza "MUNGU" huyo wasiyemjua ili asije akawakasirikia na kuwaadhibu. Ndiyo maana walijenga madhabahu hiyo kisha wakaiandika maneno "...KWA MUNGU ASIYEJULIKANA..." ili "MUNGU" huyo afahamu watu hao wanaheshimu uwepo wake ingawa hawajui kama yeye yupo.
Watu hao wa Athene walifanya ibada zao na kutoa dhabihu zao kwenye madhabahu hiyo ingawa walikuwa na hakika kuwa hawamjui yule wamtoleaye sadaka na kuwabudu. Kwa kweli hiyo ni nidhamu ya hali ya juu sana. Jambo hili linashangaza sana, hebu nikuulize swali lifuatalo:
Watu hao wa Athene walifanya ibada zao na kutoa dhabihu zao kwenye madhabahu hiyo ingawa walikuwa na hakika kuwa hawamjui yule wamtoleaye sadaka na kuwabudu. Kwa kweli hiyo ni nidhamu ya hali ya juu sana. Jambo hili linashangaza sana, hebu nikuulize swali lifuatalo:
Je! Wewe wamjua na kumfahamu Mungu unaye mwabudu, au na wewe pia unafanana na hao watu wa Athene wanaomwabudu Mungu wasiye mjua?
Kama jinsi mtume Paulo alivyo simama katikati ya Areopago na kuwaambia watu wa Athene kwamba: "...mimi nawahubiri habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua." (Mdo 17:23),
nami pia nakupasha habari njema kuwa; leo ninao ujumbe kwako kutoka kwa
Mungu wa kweli anayestahili pekee kuabudiwa. Fatilia kwa makini somo
hili nawe utabarikiwa na kufunguka ufahamu wako kwa kuitambua imani ya
kweli iwezayo kukufikisha mahali pasipo na majuto ya milele.
Zingatia kwamba: Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapo ikubali kweli.
Zingatia kwamba: Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapo ikubali kweli.
Vile vile Biblia Takatifu ilipoandika "...Paulo akasimama katikati ya Areopago...", neno "Areopago" linamaanisha "baraza kuu la Waathene, au mahali pa kukutania (mahali pa kufanyia mikutano)."
c): Kundi la watu wale wanaosema wanaye mmoja wanayemwabudu. Wakidhani wanamwabudu Mungu wa kweli, kumbe wamepotea na wanazidi kupotea kwa kutoijua kweli.
c): Kundi la watu wale wanaosema wanaye mmoja wanayemwabudu. Wakidhani wanamwabudu Mungu wa kweli, kumbe wamepotea na wanazidi kupotea kwa kutoijua kweli.
Watu wa kundi hili ni vipofu wa rohoni japo kuwa miili yao inayo macho ya nyama. Wao wanasema wanamwabudu Mungu mmoja. Ni kweli kuwa Mungu ni mmoja. Lakini leo napenda nikufunulie siri hii yawezekana haukuijua awali; Biblia Takatifu inasema kwamba:
"Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka." (Yakobo 2:19)Kuamini kwako tu si kitu kwa maana hata mashetani nao wanaamini kama jinsi ambavyo wewe unaamini; tena wewe unazidiwa na mashetani kwa sababu wao wanatetemeka kwa kuwa wanamjua Mungu wa kweli aliyewaandalia hukumu ya milele, wakati wewe humjui Mungu wa kweli. Kuamini kwako si kitu. Imani haiishii tu katika kusema unamwabudu Mungu mmoja; ni lazima ujue, je! Ni nani huyo unaye mwabudu?
Katika kundi hili la watu wanaoamini kwa kupapasa (vipofu wa rohoni) nao wamegawanyika katika matabaka mbali mbali ambayo nao wanapishana katika yule wanaye mwabudu. Watu wengi wakifika katika hatua hii, wengi wao huchanganyikiwa kwa kushindwa kuifahamu kweli. Nasema hivyo kwa sababu hapa ndipo palipo na njia nyingi ambazo zinaleta upinzani dhidi ya ile njia ya kweli kiasi kwamba wapo watu washindwao kuijua kweli kutokana na upinzani huo.
Bila shaka yawezekana si jambo geni kusikia neno "dini" (njia) na neno "madhehebu" (makundi) mbali mbali yanayo hubiri habari za Mungu hapa duniani. Lakini, kitu cha kushangaza utaona kila kundi (dhahebu)na kila njia (dini) inayo mafundisho tofauti na hilo kundi jingine; na tena makundi hayo yote hayaelewani, hayasikilizani, hayaabudu pamoja, na wala hayaheshimiani kwa kuwa kila kundi linamwona mwenzake amepotea. Kama sote tunaamini Mungu yupo; tena sote tunasema kuwa tunamwabudu Mungu mmoja; je! Utengano huu unatoka wapi? Kwa vyo vyote vile lazima hapa lipo tatizo kubwa sana. Jambo hili tunapaswa kulichukulia umuhimu na umakini mkubwa mno. Nakumbuka ipo hadithi niliyowahi kusimuliwa na baba yangu, aliniambia hivi:
"Siku moja Shetani na rafiki yake walikuwa katika matembezi, rafiki wa Shetani akawa anamwambia Shetani kwamba: 'Unasikia kila tunapopita watu wanavyosema? Mara huyo Allah akubaru; Huyo, Yesu asifiwe; Yule, Tumsifu Yesu Kristo; Wengine, Uhuru wa Yesu; n.k. Lakini sijasikia hata mtu mmoja akilisifu jina lako Shetani. Inaonekana wewe Shetani umeshindwa kazi yako.' Kisha Shetani akamjibu huyo rafiki yake kwamba: 'Ni kweli kuwa watu hao hawalitaji jina langu wazi wazi, lakini je! Kati yao umeona wanaumoja au wanaelewana? Mimi nimekwisha maliza kazi yangu hata kama wao hawanitaji jina langu.'"
Huo ndio ukweli. Shetani amekwisha maliza kazi yake kwa kuweka mafundisho mengi ya uongo. Ni lazima tuitafute kweli ilipo ili tusije tukapotea. Leo ninayo habari njema kwako: Mungu muumba wa vyote anataka afungue fahamu zako na akili zako ili uijue imani ya kweli, na uibaini pia imani ya uongo ili ujiepushe nayo. Lakini zingatia kwamba: Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapo ikubali kweli.
Humu duniani zipo dini (njia) nyingi sana; Miongoni mwa njia (dini) hizo, zipo ambazo zinawafuasi wengi na baadhi hazina wafuasi wengi. Katika dini zilizopo; kuna Wayahudi, Wabudha, Washinto, Wahindu, Wabaniani, Waislamu, Wakristo, n.k. Miongoni mwa hizo nilizotaja zipo mbili tu ambazo zinao wafuasi wengi ambazo ni: (i) Wakristo; na (ii) Waislamu. Na hawa wote wanavyo vitabu vya imani zao ambavyo vinatofautiana kwa mafundisho. Pia, kila mmoja wao anamwona mwenzake amepotea. Je! Miongoni mwao ipi ni iliyo imani ya kweli?
Hebu kuwa makini hapa; nataka tujifunze kwa kina kwa kuichambua imani moja baada ya nyingine kati ya hizo mbili ili tuweze kuibaini kweli ipo wapi. Tafadhali usichoke. Chukua kalamu na daftali lako ili uwe unanakiri pointi za muhimu kwako kwa kujisomea. Lakini zingatia kwamba: Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapo ikubali kweli.
A: IMANI YA UISLAMU.
Katika imani hii wao wanaamini ya kuwa Mungu ni mmoja na wanamtambua kwa
jina la "Allah". Wanaamini kwamba "Allah" hajazaa wala kuzaliwa, na pia
hana mshirika kwenye "Uungu" wake.
Imani hii ya Uislamu ilienezwa na mtume wao ajulikanae kwa jina la
"Muhammad (s.a.w)", na pia wao husadiki kwamba Uislamu ulianzia tangu
kwa Adamu ambaye ni mtu wa kwanza kuumbwa. "HUKO MBELENI TUTAJIFUNZA ASILI NA CHIMBUKO LA IMANI YA UISLAMU PAMOJA NA KUENEZWA KWAKE."
Wao Waislamu wanatumia "Qur'an" ambayo ndiyo kitabu chao kitukufu, wanaamini vitabu vyote vitakatifu hushushwa kutoka mbinguni, kwa hiyo "Biblia Takatifu" ilishushwa na Mwenyezi Mungu kabla ya kitabu cha Qur'an. Japokuwa wao wamewatenga Wakristo kwa kuwaona wanapotea, lakini nao Waislamu si wamoja kwa sababu ndani yake upo utengano na wanatumia Qur'an za aina mbili ambazo zinapishana; ipo ya Wasuni, na pia ipo ya Washia ambazo zinapishana juzuu ndani yake. Hivyo tunakuta napo ndani ya imani hii pia yapo matabaka yanayopingana. Je! Hapa usalama upo?
Wao Waislamu wanatumia "Qur'an" ambayo ndiyo kitabu chao kitukufu, wanaamini vitabu vyote vitakatifu hushushwa kutoka mbinguni, kwa hiyo "Biblia Takatifu" ilishushwa na Mwenyezi Mungu kabla ya kitabu cha Qur'an. Japokuwa wao wamewatenga Wakristo kwa kuwaona wanapotea, lakini nao Waislamu si wamoja kwa sababu ndani yake upo utengano na wanatumia Qur'an za aina mbili ambazo zinapishana; ipo ya Wasuni, na pia ipo ya Washia ambazo zinapishana juzuu ndani yake. Hivyo tunakuta napo ndani ya imani hii pia yapo matabaka yanayopingana. Je! Hapa usalama upo?
Waislamu wanayakubali baadhi ya mafundisho na maandiko matakatifu yaliyomo ndani ya Biblia Takatifu ambayo ni "Injili, Torati, na Zaburi", wakati huo huo wanayakataa mafundisho yote mengine yaliyomo ndani ya Biblia Takatifu.
Japokuwa Waislamu wanayapinga na kuyakataa mafundisho mengine yote
yaliyomo ndani ya Biblia Takatifu isipokuwa "Injili, Torati, na
Zaburi"; ndugu mpendwa ufatiliaye somo hili, hebu tutazame; Je! ni
kweli Waislamu wanaishika "Injili, Torati, na Zaburi" kama jinsi
ambavyo wao wanavyodai?
Katika imani hii wanaamini Mungu yupo katika Utatu Mtakatifu; yaani,
Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu. Mwanzilishi wa imani
hii ni Bwana Yesu Kristo.
Chagua somo hapo chini na ubonyeze ili uweze kufungua huo ukurasa na uendelee kusoma.
KARIBU ! ! !
- Somo: IMANI YA UKRISTO. (bonyeza hapa)
- Somo: IMANI YA UISLAMU. (bonyeza hapa)
Zingatia kwamba:
"Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapo ikubali kweli." - na: Mwinjilisti Masanja Sabbi.
Nakutakia baraka tele kutoka kwa Mwenyezi Mungu pindi uendeleapo kujifunza neno Lake.
Wakristo
wote wanatumia Biblia Takatifu ambayo ndiyo kitabu kitakatifu kwao.
Kwenye imani hii pia kuna matabaka mbalimbali (madhehebu) ambayo
tutajifunza kwa kina huko mbeleni katika somo hili.
Baada ya kupata maelezo hayo ya awali kuhusu matabaka hayo ya imani,
bila shaka utakuwa umepata mwanga japo kwa mbali kuhusu imani hizo. Sasa
basi, hebu tujifunze; Je! Kati ya imani hizo ni ipi iliyo imani ya kweli wanaomwabudu Mungu wa kweli?
Zipo namna kuu mbili za kutofautisha imani ya kweli na imani ya uongo, nazo ni hizi zifuatazo:
i/: Kutazama uwepo na asili ya imani, pamoja na asili ya yule wanayemwamini.
ii/: Kutazama nguvu na uweza wa yule wanayemwamini.
Katika kujifunza kwetu tutazingatia pointi hizo mbili kwa kuzitazama kwa
kina ili tupate kuibainisha imani ya kweli. Tutajifunza kwa kina kuhusu imani ya Ukristo, pamoja na imani ya Uislamu kwa kuwa hizo ndizo imani mbili zenye mvutano mkubwa hapa ulimwenguni. Napenda tuanze kujifunza ifuatavyo:
Chagua somo hapo chini na ubonyeze ili uweze kufungua huo ukurasa na uendelee kusoma.
KARIBU ! ! !
- Somo: IMANI YA UKRISTO. (bonyeza hapa)
- Somo: IMANI YA UISLAMU. (bonyeza hapa)
Zingatia kwamba:
"Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapo ikubali kweli." - na: Mwinjilisti Masanja Sabbi.
Nakutakia baraka tele kutoka kwa Mwenyezi Mungu pindi uendeleapo kujifunza neno Lake.
Asante kwa kutembelea matendomgeni.blogspot.com
1 comments
Umejitahidi kuandika bahati mbaya kichwani umejaa hewa....huelewi unaandika nini pole sana.
Post a Comment