Wazee
wetu walishawahi kuneno kwamba; Ukishangaa ya Mussa utayaona ya
filauni! Ndivyo unavyoweza kuanza kusema kuhusiana na tukio la
kushangaza lililotokea Kijiji cha Udindila Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa
Pwani.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT aliyetambulika kwa jina la Boniface Onesmo
alijikuta akibubujikwa na machozi mara baada ya kushuhudia mkewe Bi.
Benta Boniface akijifungua hirizi baada ya kushika mimba kwa kipindi cha
miezi saba na nusu!
Akizungumza na mtangazaji wa Kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm,
Edson Mkisi Jr, Mchungaji huyo alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo
mkewe amekuwa na matatizo ya kuharibika kwa mimba za mara kwa mara na
tangu kuhamia kwa eneo hilo la Udingila Bagamoyo mkewe huyo hajawahi
kuzaa mtoto hata mmoja angawa amekuwa akishika mimba kila walipohitaji
kuzaa.
“Kwa hakika Mungu ni mwema na sitaacha kuendelea kumsifu na kumuabudu,” alianza kueleza Mchungaji Onesmo.
“Zaidi ya mtoto huyu mmoja niliyemzaa kabla ya kuhamia hapa, hivi sasa
kila ninapotaka kuzaa mtoto mimba za mke wangu zinaharibika na hadi muda
huu mimba zaidi ya nne zimeshaharibika nah ii nyingine ndio amezaa
hirizi!” Mchungaji Onesmo alisimulia.
Mwandishi wa times akihojiana..
Aliezeza kuwa siku ya tukio, mkewe kipenzi alianza kusikua uchungu tangu
saa nne asubuhi na kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo uchungu
ulipozidi kuongezeka.
“Hali iliendelea hivyo hadi saa nne usiku ambapo mkewe alihisi kabisa
kupushi na mimi nilikuwa tayari kumsaidia lakini wakati anaendelea
kupushi mkewangu akawa anatoa haja ndogo mara kwa mara na alitoa haja
ndogo hadi ndoo nne ndogo zilijaa na kumwaga nje.
“Baada ya hapo aliendelea kusikia maumivu makali ya tumboni huku akihisi
kuzaa lakini baadae aliposikia mtoto anakuja na mimi kujiweka tayari
kumzalisha niliona kitu kinatoka kama mtoto kukivuta ikatoka hirisi
ikiwa imefungwa kitambaa chenye rangi chekundu na nyeusi!” anasema.
Aidha, kwa upande wa mkewe, alisema kama siku hiyo kungekuwa na sumu ya panya angekunywa afe akapumzike.
Akizungumze huku akilia, mama Dotto (Benta), anasema siku ya tukio hilo
roho yake ilinusa kaburi kama kungekuwa na hata mafuta ya taa
kwenye kopo angekunywa ili afe.
“Nilimuuliza mume wangu mara kadhaa kama kwenye kopo kuna mafuta ya taa
lakini aliniambia yote aliweka kwenye kandiri (taa ya chemli) na hata
nilipoangalia tunapoweka sumu sikuiona….kwa hakika kama ningekiona
kimoja wapo ningekunywa nife! Nimeteseka sana,” anasema mama Dotto.
Mama Dotto alisema pamoja na changamoto zote anazokutana nazo Bagamoyo
lakini hajafikiria wala hafikirii kwenda kwa mganga wa kienyeji.
Nukuu “Siwezi kwenda kwa mganga wa kienyeji kwa sababu waganga ukienda wao
huongeza tatizo kwa hiyo nitaendelea kumuomba Mungu hadi atakaposikia
maombi yangu,” anasema huku akiangalia na mumewe pamoja na majirani
waliofika kumjulia hali.
Habari kwa hisani ya www.timesfm.co.tz
Tuesday, August 26, 2014
AMA KWELI MGANGA HAJIGANGI MKE WA MCHUNGAJI KUJIFUNGUA HIRIZI! DUH! SOMA HAPA..
Posted by
Unknown
at
2:18 PM
Tags :
0 comments
Post a Comment