Saturday, April 12, 2014

RUNGU LA YESU PASAKA UNYAMWEZINIIII!!!!....SOMA HAPA UJUE YESU OKOA MITAA ITAKUA WAPI PASAKA HII?......

Mwanaharakati na jemedari wa yesu RUNGU LA YESU ambaye ni moja kati ya waasisi wa harakati za yesu okoa mitaa kila kona ya mtaa, blog hii imepata nafasi ya kufanya mahojiano naye hasa kutaka kujua pasaka hii harakati hizo zitakua wapi? 
                      SOMA NUKUU CHINI HAPO..
                                                         
 Akiwa na wanaharakati wengine wakwanza kulia ni martin  bashando
                               Rungu katika pozz la kiroho
             Rungu la yesu na mwana hiphop briyan mwimba
 Rungu la yesu na wanaharakati akiwemo man warter wa 3 kulia
                                     Nukuu

Nimepata safari ya kwenda Unyamwezini  na safari hii sio tuu kwenda kula pasaka la hashaa safari hii itakua na mambo makubwa sana na ya msingi mno yakiwa yamebebwa na slogani yetu ya yesu okoa mitaa kila kona ya mtaa, nitakua TABORA kuanzia tar 16 april jumatano hadi tar 20 april jumapili ambapo ndio pasaka pale FPCT BOMBA MZINGA nitakua nikifundisha neno la Mungu pale kanisani lakini jumapili hiyo ya pasaka jioni kutakua na boooonge la tamasha la yesu okoa mitaa kila kona ya mtaa. Niwaombe tuu wakazi wa Tabora na maeneo ya karibu wafike kwenye semina hiyo ambayo itawafanya warudi wakiwa wame ongeza vitu vingi na kujifunza meengi, lakini kwa msisitizo siku ya juma pili ndio kabisaaa hapatatosha pale kwa tamasha ambapo mpaka sasa maandalizi yameshakua mazuri kwa asilimia 97% karibuni sana sana sana kanisani  FPCT BOMBA MZINGA pale Tabora mjini kwa mtumishi wa Mungu DAVID AMON. Nawatakia kila la kheri na sikukuu njema ya pasaka. YESU OKOA MITAA KILA KONA YA MTAA.
                                             MWISHO WA KUNUKUU.


Alimaliza kwa kusema hivyo Mwanaharakati huyu machachali wa kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji kwa style ya hip hop.
Kutoka http://matendomgeni.blogspot.com   Tunamtakia harakati njema na Mungu awabariki wooote wanao surport harakati hizi popote walipo Mungu awabariki saana.



0 comments

Post a Comment