Monday, September 1, 2014

HARAKATI ZA KUMTIMUA SHETANI ZINAENDELEA NI KONA HADI KONA SOMA HAPA....

Baada ya kuachia nyimbo yake kari ya kuwashauri vijana wawapende wazazi wao sasa ameachia nyimbo nyingine ambayo kwa hakika kila siku amekua akifanya vizuri saana anapo achia nyimbo zake huyu ni BASHANDO, ambae pia kwa utafiti tulio ufanya matendomgeni.blogspot.com tumebaini kua ndiye gospel hip hop raper ambaye yupo wise sana kwenye huduma yake na maisha yanayo mhusu na ndie aliye karibu saana pia na mitandao ya kijamii hususani facebook lakini pia anaongoza kwa ku show love kwa mwanae kwa ku post sana picha zake, nilipo kua na mahojiano nae nikimuuliza ni changamoto gani alizo kutana nazo kabla hajawa bashando na zile anazo kutana nazo kwa sasa alikua na haya ya kusema 
             Sikiliza nyimbo yake hii mpya NYENYEKEA

                                         NUKUU.

Pamoja na kuanza kufanya Gospel Hip Hop miaka mingi sana iliyopita lakini sijipi uhakika kuwa mimi ndiyo muhasisi, ila tu ninamshukuru Mungu kwa uzoefu nilioupata kupitia matusi, kejeli, kutengwa na kudharaulika, ambavyo ndio vitu vilivyonifanya kuwa Bashando ninaeonekana leo hiii. Kuna wakati nilikuwa nasoma nyaraka ya mtume Paulo alipoandika kua neema ya Mungu inakamilika katika mapungufu yake, lakini sikuwa najua dhahiri ni kitu gani alichokuwa anakimaanisha ila sasa nimeweza kujua, na ninazidi kumshukuru Mungu kwa mapito yote niliyopitia bila kujari yaliniumiza kiasi gani.
Wengi wakiniona stejini leo naimba wanatamani kuwa kama mimi ila sidhani kama nikiwashirikisha kikombe nilichokinywea hadi kufika hapa kama wanaweza kutamani kukishiriki pamoja nami, ila yote katika yote Mungu ni mwema. Kupitia nyimbo hiiutaweza kugundua kuna ukomavu wa aina gani na ninahisi kwa mtu makini ataelewa kuwa tumeitwa kufanya kazi hii na wala hatujajiita, na kama tumeitwa bosi wetu hawezi kutuangusha maana ofisi ni yake, na sisi ni watenda kazi tu. 
                                 MWISHO WA NUKUU.
                                          Bashando akihudumu
                                            Muonekano wa mwanae
                                       Mtoto aki enjoy maisha ya baba na mama

                              Bashando na mwanae
0 comments

Saturday, August 30, 2014

MWANA GOSPEL HIP HOP ASEMA USHIRIKIANO BADO NI DHAIFU TANZANIA! MUNGU TUSAIDIE!

Mwana gospel hip hop Tanzania ambaye aliingi katika tuzo za AGMA africa gospel award amesema tuzo sijapata lakini najua kwanini sijapata, unajua watanzania kuna kitu kinaitwa uzalendo siku zote hatuna na kwenye upande wetu wa Gospel pia kuna kupendana kwa kinafiki kwa sababu haiwezekani moja ya mtandao wa kijamii mkubwa unao uamini kwamba utaku surport kwa kuwapelekea jamii taarifa juu ya kuwepo kwako kwenye tuzo, mtandao huo unakuja ku post habari hiyo siku moja kabla ya upigaji wa kura kuisha, sasa huu kama sio unafiki ni nini? yaani ni sawa na mtu anakuja kuchangia kwenye msiba mihela mingi wakati unapo umwa uliomba msaada hakukusaidia, { GAZUKO alisema} wito wangu kwa jamii hasa hii ya kikristo ni kwamba tusidhani trip zetu za kwenda kanisanni ndio hasa zitatupeleka kwenye uzima wa milele bali ni upendo wa dhati kwa ndugu jamaa na marafiki zetu haijalishi wao wana mapungufu gani, kwani hii ndio amri kuu. NI HAYO TUU, akiongelea muendelezo wa harakati zake na YOM kwa ujumla alisema jamii ikae mkao wa kula kupitia YOM project kuna video kali, movie kali na mengine meengi ambapo camera ambayo walizawadiwa siku ya mwaka mmoja wa YOM pale tabata inahusika saana.
 Gazuko akiwa na Edson Mwasabwite studio kufanya nyimbo mpya! {Ombi langu}
                           Gazuko na mkari wa nyimbo za injili
 Moja ya matangazo yaliyo kua yakiwataalifu watu wapige kura..
                         Rungu la yesu,Bashando na Gazuko.

           Gazuko aki jadili kitu na mkari BASHANDO
0 comments

Wednesday, August 27, 2014

KIMBILIO JIPYA LA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI HILI HAPA!

Ikiwa umitimia mwaka mmoja sasa toka harakati za wana yesu okoa mitaa YOM kuanzishwa moja ya mafanikio tuliyo yapata ni kuokolewa kwa watu sehemu mbalimbali sababu ikiwa ni kwa huduma yetu ya uimbaji, haya yamesemwa na mmoja wa wanaharakati ambao hasa ndio mstari wa mbele kuhakikisha kwamba shetani ana kula za uso mpaka ana sanda, jumapili ya tar 24 augost 2014. tulikua tunatimiza mwaka mmoja toka kuanzishwa kwa huduma yetu ambayo kimsingi imefanikiwa saana kwasababu tumekua na wadau ambao wana tu surpot sana iwe kwa hali na mali, hatuwezi kuwataja wote wanao tu surport lakini Mungu anawajua na tunawaombea saana, lakini nitoe shukrani zangu nyingi kwa niaba ya wana YOM wote kwa mh:Katibu mkuu wa TAG Rev Roni Swai ambae pia ndio mlezi wetu, kwa. lakini Mungu ni mwema saana kwani mtumishi wa Mungu COSATO CHUMI kwani alitufanyia surprise ya kutuzawadia camera aina ya SONY {div}cam yenye thamani ya Tsh 12,000,000/= milioni kumi na mbili. ilikua shangwe na vigeregere saana. hayo yalikua maelezo ambayo ali tiritirika Mtumishi wa Mungu RUNGU LA YESU pale nilipo fanya na e mahojiano, aliendelea kwa kusema kwasasa tumefikia sehemu nzuri saana tafauti na mwanzo ambapo watu wengine walikua wakibeza huduma yetu lakini sasa unaona Mungu wetu anajibu maombi yetu kwa sababu kupata camera hii ndio mwanzo wa kufikia malengo yetu ya kufikisha huduma yetu mbaali zaidi, kwa hiyo kwa sasa ni kazi kwetu kufanya Audio songs nzuri zenye ubora na baadae kufanya video ambapo tayari camera tunayo ooooh haleluyaaaa! alisema. Mwisho akasema watu wanatakiwa wajue kwamba YOM sio ya mtu fulani YOM ni ya kila mtu anae mjua Mungu na yupo tayari kumtangaza yesu kwa njia ya uimbaji film n.k kwani kwa sasa mpango wetu ni pamoja na kufanya film kwahiyo kwa yeyote atakaye hitaji kufanya kazi na sisi iwe song video au film awasiliane kupitia blog hii au tembelea ukurasa wetu wenye jina la YESU OKOA MITAA TZ. ASANTE.

                                            Kamera iliyo tolewa
                         Masanja pia alikuwepo kutoa surport
               Rungu la yesu akishukuru kwa niaba ya wana YOM
                               Emmanuel mbasha pia alikuwepo.
                                      Masanja kama kawaida yake .. akifanya yake
                                    Mlezi wa YOM mtumishi SWAI.
0 comments

Tuesday, August 26, 2014

AMA KWELI MGANGA HAJIGANGI MKE WA MCHUNGAJI KUJIFUNGUA HIRIZI! DUH! SOMA HAPA..

Wazee wetu walishawahi kuneno kwamba; Ukishangaa ya Mussa utayaona ya filauni! Ndivyo unavyoweza kuanza kusema kuhusiana na tukio la kushangaza lililotokea Kijiji cha Udindila Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Mchungaji wa Kanisa la EAGT aliyetambulika kwa jina la Boniface Onesmo alijikuta akibubujikwa na machozi mara baada ya kushuhudia mkewe Bi. Benta Boniface akijifungua hirizi baada ya kushika mimba kwa kipindi cha miezi saba na nusu!



Akizungumza na mtangazaji wa Kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Edson Mkisi Jr, Mchungaji huyo alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo mkewe amekuwa na matatizo ya kuharibika kwa mimba za mara kwa mara na tangu kuhamia kwa eneo hilo la Udingila Bagamoyo mkewe huyo hajawahi kuzaa mtoto hata mmoja angawa amekuwa akishika mimba kila walipohitaji kuzaa.

“Kwa hakika Mungu ni mwema na sitaacha kuendelea kumsifu na kumuabudu,” alianza kueleza Mchungaji Onesmo.

“Zaidi ya mtoto huyu mmoja niliyemzaa kabla ya kuhamia hapa, hivi sasa kila ninapotaka kuzaa mtoto mimba za mke wangu zinaharibika na hadi muda huu mimba zaidi ya nne zimeshaharibika nah ii nyingine ndio amezaa hirizi!” Mchungaji Onesmo alisimulia.

                      Mwandishi wa times akihojiana..

Aliezeza kuwa siku ya tukio, mkewe kipenzi alianza kusikua uchungu tangu saa nne asubuhi na kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo uchungu ulipozidi kuongezeka.

“Hali iliendelea hivyo hadi saa nne usiku ambapo mkewe alihisi kabisa kupushi na mimi nilikuwa tayari kumsaidia lakini wakati anaendelea kupushi mkewangu akawa anatoa haja ndogo mara kwa mara na alitoa haja ndogo hadi ndoo nne ndogo zilijaa na kumwaga nje.

“Baada ya hapo aliendelea kusikia maumivu makali ya tumboni huku akihisi kuzaa lakini baadae aliposikia mtoto anakuja na mimi kujiweka tayari kumzalisha niliona kitu kinatoka kama mtoto kukivuta ikatoka hirisi ikiwa imefungwa kitambaa chenye rangi chekundu na nyeusi!” anasema.

Aidha, kwa upande wa mkewe, alisema kama siku hiyo kungekuwa na sumu ya panya angekunywa afe akapumzike.

Akizungumze huku akilia, mama Dotto (Benta), anasema siku ya tukio hilo roho yake ilinusa kaburi kama  kungekuwa na hata mafuta ya taa kwenye kopo angekunywa ili afe.

“Nilimuuliza mume wangu mara kadhaa kama kwenye kopo kuna mafuta ya taa lakini aliniambia yote aliweka kwenye kandiri (taa ya chemli) na hata nilipoangalia tunapoweka sumu sikuiona….kwa hakika kama ningekiona kimoja wapo ningekunywa nife! Nimeteseka sana,” anasema mama Dotto.

Mama Dotto alisema pamoja na changamoto zote anazokutana nazo Bagamoyo lakini hajafikiria wala hafikirii kwenda kwa mganga wa kienyeji.

Nukuu  “Siwezi kwenda kwa mganga wa kienyeji kwa sababu waganga ukienda wao huongeza tatizo kwa hiyo nitaendelea kumuomba Mungu hadi atakaposikia maombi yangu,” anasema huku akiangalia na mumewe pamoja na majirani waliofika kumjulia hali.


Habari kwa hisani ya www.timesfm.co.tz


0 comments

Monday, August 25, 2014

YESU OKOA MITAA BIRTHDAY YAFANA PETER BANZI AONGELEA SIRI YA MAFANIKIO YAKE SIKILIZA HAPA & ANGALIA PICHA

Ni mwaka mmoja wa harakati za Yesu okoa mitaa al maarufu kama YOM iliyo fanyika jumapili ya tar 24/8/14 pale Tabata DCT. ilikua siku nzuri saana kwa tulio hudhulia hasa pale wana harakati walipo fanya yao stejin ambapo VEE JAY alifungua dimba na wengine kuendeleza jaramba hilo lakini baada ya v jay peter banzi alipokea kijiti cha kumkimbiza shetani eneo lile hapo ndipo umati wa watu ulio kuwepo ndani ulilipuka kwa shangwe na kucheza nae kwa furaha kubwa, hapo ndipo alinifanya nisimame na kwenda kumuhoji nini siri ya kufanikiwa kwake siku hii, wengine walio fanya vema ni pamoja na BASHANDO, RUNGU LA YESU NICKODEMUS SHABOKA, MNENE MAKWETA, mwanadada BEATRICE, na wengine weengi sana MC akiwa MC RAULENCE MWATIMA siku hiyo ilifana saana chini ya mshereheshaji huyo makini na mwenye mbwembwe nyingi. sikiliza hapa chini alicho ongea PETER BANZI NA MANAGER WAKE...
                           Mwana dada Beatrice mwana gospel hip hop
 Nickodemus shaboka ni hatareee sana huyu mutu ya Mungu! akiwa na Vee jay!
 Huyu ni mhudumu pale Nchi ya ahadi kwa mchungaji Harris kapiga! his name TONNY..
 Mwana Gospel ambaye alikua tofauti na mtu yeyote siku hii kwa uvaaji wake was Amaizing!
 Gospel singer from KENYA akiwa na director wa video ya acha kulia ya Gazuko alikuwepo akitokea U.S.A
 Mdau mkubwa saana wa mziki wa injili bongo huitwa Diana Natasha akiwa na Gazuko junior.
                                                         Wana harakati wa YOM
 Mtoto mdogo saana akifanya yake stejin kaazi kweli kweli shetani aliaibika kweli yaani
 Novic ni mkari saana wa flow allthe way from glean city mpaka Dar
 Kubwa la maadui katika safu ya mbele ya kumuangamiza shetani RUNGU LA YESU..
 Sumu za kumteketeza shetani katika kitengo cha uchezaji maduku n.k (T- shert ya blue ni Gazuko..)
 Huyu ndio star wa siku PETER BANZI wa kwanza kulia akiwa na meneja wake..
                Waku shoto ni PETER BANZI MANAGER
                     Kifaa kingine kutoka YOM BASHANDO..
 HOPE HUYU KIJANA NI SHEEEDA pia ni BLOG CREATER...
                  Baraaaaa! shetani mikono juuuuu juuuuu!
            Umati wa watu waki shuhudia kipigo cha shetani live!
0 comments

Saturday, August 23, 2014

UCHAWI WAHUSISHWA KWENYE MZIKI WA INJILI SIKILIZA HAPA....

Gazeti la risasi la tar 2 augost 2014 Rais wa muziki wa injili tanzania aliongelea baadhi ya matukio yaliyo tokea mwaka huu kwenye Gospel industry, kwamba uchawi unaweza kua ndio chanzo cha ajari na vifo vilivyo tokea. akizungumza na waandishi wa habari wa kampuni ya gloubal publishers Rais wa waimbaji wa mziki wa injili tanzania mh: ADDO NOVEMBER ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo hizo alisema kwenye msafala wa mamba kenge pia wamo akimaanisha kwamba vifo na ajari zinazo tokea kwa waimbaji wa gospel uchawi unahusishwa japo hakufafanua kwamba waimbaji kwa waimbaji ndio wana logana au laa! alicho sema ni kwamba kuna taarifa kwamba kuna watumishi wa Mungu ambao inasemekana kwamba hua wana enda nigeria kutafuta dawa za kuwasaidia kufanya huduma kwa kupendwa zaidi na jamii! sasa sikiliza hapo chini alicho kisema mwana gospel Makini saana anaye kwenda kwa jina la Matendo Andrew, juu ya imani hizo za kishirikina na huduma za KI Mungu, mwana gospel huyu ambaye kabla ya mwaka huu kuisha anatarajia kuingiza sokoni album itakayo kua na nyimbo ishilini (audio) na video 9 au 10, anasema hii ni kwa mara ya kwanza tanzania haijawahi kutokea lakini yeye anahitaji kuonyesha uwezo wake na ukomavu wake katika kumjua Mungu kwa kufanya hivyo,..... USIKOSE KUTEMBELEA HAPA matendomgeni.blogspot.com kwa habari za Gospel industry na mengine meengi pia usisite kuwasiliana nasi kwa number hizo hapo juu na imail hii matendoandrew@gmail.com.


                                                      ADDO NOVEMBER
 Paraglaf iliyo kua na habari ya Addo november juu ya UCHAWI

                                             ADDO
                       Mwonekano wa gazeti hilo kwa nje
0 comments

Friday, August 22, 2014

SIKILIZA HAPA ALICHO SEMA MWANA GOSPEL HUYU JUU YA EDSONI MWASABWITE NA BONY MWAITEGE.. NI SHEEEEEDA!!!

Mwimbaji wa nyimbo za injiri Matendo Andrew ambaye pia ndio mmiriki wa blog ya matendomgeni.blogspot.com amefunguka mengi juu ya uzembe wa baadhi ya wanamziki wa nyimbo za injiri kutokua karibu na mitandao ya kijamii akiwatolea mfano BONY MWAITEGE NA EDSON MWASABITE
msikilize hapo alicho kiongea..
              Edson Mwasabwite studio akipiga picture
 Bonny Mwaitege akifanya tendo ambalo ni gumu saana kwa vijana wengi wa sasa.
                 Matendo Andrew The gospel singer him self
                                   Matendo Andrew
                     Moja ya cover za album za Bony mwaitege
             Audio cover ya album ya pili ya Edson mwasabwite.
0 comments

Thursday, August 21, 2014

NI MARA NGAPI UMESIKIA TETESI ZA UTAPELI WA ROSE MUHANDO ? SOMA HAPA HALAFU JIONGEZE...


ROSE MUHANDO KATIKA POZI

Ile habari iliyoandaikwa na Moja ya magazeti yanayotoka mara moja kwa wiki kuwa muimbaji wa nyimbo za Injili Rose Muhando alifikishwa kituo cha polisi kwa utapeli, sasa ukweli wake wajulikana.
Akizungumza na Mtandao wa MO Designtz, Producer au mtayarishaji wa muziki anayetengeneza nyimbo za Rose Muhando Enock Nyongoto au Producer Eck, amesema kuwa Rose Hajafikishwa kituoni ila yeye ndiye aliyekwenda kituoni na si Rose.

PRODUCER ECK AKIFANYA MAMBO YAKE
Producer Eck anasema kuwa kisa cha yeye kupelekwa polisi baada ya Rose kutopatikana, ni kuwa wakati Rose anakabidhiwa pesa yeye alikuwepo na yeye alikuwa kama shahidi. " wakati Rose anakabidhiwa pesa na kuandikishana na huyo mchungaji mimi nilikuwa kama shaidi na ndio maana polisi walinifuata mimi baada ya kumkosa Rose muhando." alisema Producer Eck.
akihadidhia kisa kizima kilivyokuwa Producer Eck alisema kuwa Baada ya Rose kukabidhiwa pesa kwa makubaliano ya kwenda kuimba huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mji wa Bunia, Rose alijikuta akiwa na wakati mgumu sana kwani Kampuni anayofanya nayo kazi ambayo ni kampuni ya Msama Promotion walikuwa tayari walishaandaa matamasha na ambayo yalikuja kwa kufuatana hivyo akajikuta kuwa yale maandalizi tu yanaingilia ratiba zingine zote kwa vile alitakiwa kufanya mazoezi mazito kwa ajili ya kuimba live. akaendelea kusema kuwa mazoezi hayo yalikuwa mazito kwani Rose hakuwahi kuimba live hivyo akajikuta ana kazi kubwa ya kufanya mazoezi na wanamziki watakaompigia live hivyo hakuweza kabisa kwenda Congo na ukizingatia kuwa Pesa waliokubaliana na huyo Mchungaji wa Congo haikutolewa hata nusu yake.
Produce Eck anasema kuwa, Rose na huyo Mcgungaji walikubaliana kiasi cha Dola za kimarekani 5,000$ ambayo ni sawa na Shilingi milioni 8 lakini alipewa advance ya shilingi milioni 3.

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA MSAMA PROMOTION ALEX MSAMA
Akiendelea kuzungumza na MO Designtz Producer Eck anasema makubaliano hayo yalifanyika katika studio yake wakati Rose alipokuwa akimalizia kuandaa Albamu yake mpya.
Eck anasema kuwa Rose hakufanya makusudi na wala hakuwa na nia ya kufanya kama ilivyotokea. na hizi habari zilizoandikwa ni za upande mmoja kwani Rose alipokuwa akipigiwa simu alikuwa kwenye tamasha Mwanza na mara nyingi akiwa kwenye tamasha huwa hakai na simu yeye, simu wanakuwa nayo vijana wake.

ROSE MUHANDO KATIKA VIDEO YAKE YA WOLOLO
Produce Eck anasema kuwa siku ya kukamatwa, yeye alikuwa anatoka safari lakini akashangaa anapigiwa simu afike kituo chapolisi Kijitonyama Mabatini, lakini alipofika akawekwa chini ya ulinzi kwa madai kuwa yeye ndio anaweza kuwaeleza wapi kwa kumpata Rose Muhando. lakini alitolewa kwa dhamana baada ya kuongea na Mkurugenzi wa Msama Promotion ambaye alikuwa bado yuko Mwanza kwenye tamasha na akaahidi kuwa anakuja kuitowa pesa hiyo pindi atakaporudi kutoka Mwanza.
Producer Eck anaendelea kusema kuwa Msama hakusema uongo kwani leo baada ya kufika uwanja wa ndege tu kutoka Mwanza, Msama alimpigia simu Producer Eck na akamuambia akachukuwe pesa hiyo ili walipe wamalize hilotatizo. " kweli Msama alipofika tu kabla hata hajafika nyumbani kwake, alinipigia simu na kuniambia nikachukue pesa hizo kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo. Nami nilimpigia simu mchungaji tukaenda kuchukuwa hizo pesa kisha tukaenda kituo cha polisi pamoja na mchungaji kwa ajili ya kufuta jalada. hivi unavyoniona ndio nimetoka huko kituo cha polisi kwa hiyo hakuna kesi tena, na mchungaji kati ya kesho au keshokutwa anaondoka. alimalizia kusema Producer Eck.

PRODUCER ECK AKIWA NA MUIMBAJI CHIDUMULE
Habari zinasema kuwa Mchungaji huyo wa Congo ameshukuru sana kwani hakutegemea kabisa kuwa pesa hizo angeweza kuZipata ukizingatia kuwa yeye ni mgeni, hivyo anaamini kuwa kweli inawezakana Rose alikuwa hana nafasi ya kwenda Congo, akaendelea kusema kuwa hata hivyo atakwenda kuandaa tamasha ambalo litakuwa la VIP na lazima atamchukua tena Rose kwani anapendwa sana huko kwao Bunia.
Naye Rose Muhando akizungumza na MO Designtz, amesema kuwa anafahamu kuwa mashabiki wake walioko Bunia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wana hamu sana ya kumuona, hivyo anafanya mpango lazima aende kwa ajili yao na anawapenda sana.
0 comments