Sikiliza nyimbo yake hii mpya NYENYEKEA
NUKUU.
Pamoja na kuanza kufanya Gospel Hip Hop miaka mingi sana iliyopita
lakini sijipi uhakika kuwa mimi ndiyo muhasisi, ila tu ninamshukuru
Mungu kwa uzoefu nilioupata kupitia matusi, kejeli, kutengwa na
kudharaulika, ambavyo ndio vitu vilivyonifanya kuwa Bashando
ninaeonekana leo hiii. Kuna wakati nilikuwa nasoma nyaraka ya mtume
Paulo alipoandika kua neema ya Mungu inakamilika katika mapungufu yake,
lakini sikuwa najua dhahiri ni kitu gani alichokuwa anakimaanisha ila
sasa nimeweza kujua, na ninazidi kumshukuru Mungu kwa mapito yote
niliyopitia bila kujari yaliniumiza kiasi gani.
Wengi wakiniona stejini leo naimba wanatamani kuwa kama mimi ila
sidhani kama nikiwashirikisha kikombe nilichokinywea hadi kufika hapa
kama wanaweza kutamani kukishiriki pamoja nami, ila yote katika yote
Mungu ni mwema. Kupitia nyimbo hiiutaweza kugundua kuna ukomavu wa aina
gani na ninahisi kwa mtu makini ataelewa kuwa tumeitwa kufanya kazi hii
na wala hatujajiita, na kama tumeitwa bosi wetu hawezi kutuangusha maana
ofisi ni yake, na sisi ni watenda kazi tu. MWISHO WA NUKUU.
Bashando akihudumu
Muonekano wa mwanae
Mtoto aki enjoy maisha ya baba na mama
Bashando na mwanae
0 comments
Post a Comment