SKENDO ZA ROSE MUHANDO MAPYA YAIBUKA
Habari hiyo iliruka hewani kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti tumbo moja la hili, Ijumaa Wikienda la Februari 10 hadi 16, mwaka huu ikiwa na kichwa; ROSE MUHANDO MBARONI.
Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel, mara kadhaa Rose alishaingia kwenye skendo nyingi kutokana na jamaa aliyetajwa kwa jina la Nathan Wami.
Alisema katika albamu ya Rose ya kwanza kabisa iitwayo, Jipange Sawasawa alijikuta akiingia kwenye balaa la kubambikiwa msala wa kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya ambapo katika mazingira yeye utata, staa huyo alijikuta akiziachia shilingi milioni 30 bila kujijua kwa baadhi ya polisi wa Dodoma. Hiyo inadaiwa ilikuwa ‘karibisha mgeni’
Stela alifafanua kuwa, hata msala ambao ulimfikisha Rose korokoroni katika Kituo cha Polisi
cha Msimbazi Dar hivi karibuni siyo wa shilingi milioni 6 kama ilivyoelezwa awali bali ni sh. milioni 2 ambazo si yeye aliyezipokea bali ni mwanaume huyo.
Alieleza kuwa katika msala huo wa milioni 2 alizodaiwa kuchukua na kushindwa kwenda kufanya shoo Mombasa, Kenya, staa mwenzake wa Injili, Jennifer Mgendi alidaiwa kujua kila kitu alikataa kwenda Msimbazi kumtoa Rose akidai kuwa hajui chochote.
Stella alifunguka: “Tofauti na watu wanavyojua, Nathan hakuwahi kuwa meneja wa Rose bali alikuwa ni msaidizi wake tu. Kwa hiyo si kweli kusema eti Nathan aliamua kumwacha mwimbaji huyo kwa kisingizio cha kukosa mwelekeo.
“Msada pekee wa Nathan kwa Rose ni kumlipia gharama za studio alipokwenda kurekodi kwa mara ya kwanza wakati Rose akiwa anasali Kanisa la Saint Mary, Chimuli, Dodoma. Ila kama mlivyiosema kwenye gaeri la Ijumaa (Wikienda) kuna mengi yapo nyuma ya pazia.
“’Ukichaa’ wa Rose ni pale alipokosea akaenda na Nathan, Cosota (chama cha hatimiliki) na kuingia makubaliano kwa maandishi kwamba huyo Nathan ndiyo awe analipwa mrabaha (sehemu ya mapato) ya kazi zote za Rose. Ni juzijuzi tu ndiyo Rose akaniagiza mimi nikamtengulie huo mkataba,” alisema katibu huyo ambaye pia ni mwimba Injili.
Aliendelea kufafanua kuwa mikataba yote ya kazi za Rose alikuwa akisaini Nathan hadi mwimbaji huyo alipochukuliwa na lebo kubwa ya Sony inayosimamia kazi zake kwa sasa.
Akaongeza: “Kama pesa yote ingekuwa inaingia mikononi mwa Rose asingekuwa hivi alivyop leo. Fikiria mpaka sasa Rose ana gari moja tu (Toyota Prado), viwanja 3 na shamba la eka 100 pale Dumila, basi (Morogoro).”
Kwa upande wake, Rose alisema kuwa Nathan alimfanya mashine ya kutoa na kuweka fedha benki (ATM).
Nathan alipoulizwa juu ya madai yote hayo alijibu kwa sauti yenye uhakika: “Hayo madai si ya kweli. Mimi nimeishi na Rose kwa zaidi ya miaka 12. Mimi ndiye niliyemsaidia yeye. Asingekuwa alivyo sasa kama si mimi.” {KWA HISANI YA UDAKU SPECIALY}
0 comments
Post a Comment